Mama akimuaga marehemu mwanaye, Method Clecence Mengi.
MAMIA ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakiongozwa na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude wamejitokeza kumzika marehemu Method Clecence Mengi aliyeuawa kwa kuchomwa visu na watu wasiofahamika nchini Marekani.
Mengi alikumbwa na ukatili huo wa kuchomwa visu vitatu, tumboni viwili na kwenye paji la uso Septemba 17, mwaka huu nje ya nyumba yake, Texas nchini humo na watu hao bila kujulikana kisa na waliingia mitini baada ya tukio hilo la kikatili.
Mwili wa Mengi aliyeishi nchini Marekani tangu mwaka 2000, uliwasili nyumbani kwa wazazi wake, alfajiri ya Oktoba 2, mwaka huu na baadaye saa tisa alasiri kupelekwa kwenye Kanisa la Mtakatifu Patrick kwa ibada ya mazishi yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Akizungumza baada ya mazishi hayo, mdogo wa marehemu Ribbon Mkali ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilakala alisema:
Source GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment