Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Bwana mmoja jijini Mumbai nchini India, amepewa talaka yake, baada ya kulalamika kuwa hawezi kukata "kiu kubwa" aliyokuwa nayo mke wake ya kufanya tendo la ndoa.
kwa mujibu wa tovuti ya Metro - Mwanaume huyo akiwa amechoka, alifika katika mahakama inayoshughulikia masuala ya kifamilia mwezi Januari, akidai kuwa mke wake amekuwa akimnyanyasa kwa kutaka kufanya tendo la ndoa, tangu walipofunga ndoa mwaka 2012, na kuwa amekuwa akitumia 'mabavu na udikteta' wakati akitaka jambo lake. 

Na hakuishia hapo: bwana huyo ameiambia mahakama kuwa mke wake pia alithubutu hata kumpa dawa za kuongeza nguvu, na kutishia 'kutembea' na wanaume wengine kama atashindwa kukata kiu yake kubwa.
Mume huyo akiwa taabani- ambaye amesema amesumbuliwa na maradhi ya kidole tumbo 'appendicitis' kutokana na kutopumzika, alipewa talaka aliyokuwa akidai.
"Kwa kuwa mshtakiwa (mke) hakutokea mahakamani, ushahidi wa mshtaki (mume) haujapingwa. Na hivyo mahakama hii haina budi, ila kukubali ushahidi uliowasilisha" amesema Jaji Laxmi Rao.
Taarifa hii kutoka tovuti ya metro
BONYEZA HAPA

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top