Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
WASANII waliowahi kuogelea katika dimbwi zito la mahaba kisha kumwagana, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’ na Elias Barnaba ‘Barnaba Boy’, wamezua maswali mapya kwa mashabiki na kuleta tafsiri kuwa huenda wamerudiana.

Mastaa wa Bongo Fleva Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’ na Elias Barnaba ‘Barnaba Boy’ beneti.
Tukio la wawili hao kugandana kama zamani lilijitokeza juzikati walipokuwa kwenye shoo ya Serengeti Fiesta, Musoma ambapo kwenye gari walikuwa wamekaa pamoja na hata mazungumzo yao yalikuwa kama ya mtu na mtuwe.

Paparazi wetu aliyekuwa eneo la tukio alipenyezewa nyepesi juu ya ukaribu wa wawili hao, aliingia mzigoni ambapo aliwaona wako kwenye mazingira ya pamoja kila walipokuwa wakipiga misele.
Baada ya kukwepa mitego mingi ya kamera, paparazi wetu aliamua kuwauliza kama wamerudiana au laa?

Mtoto mzuri 'Shishi Baby’ akipozi.

“Hahahaaa....hebu utuache na mambo yetu bwana maana tunajua wenyewe tunachokifanya, kuachana au kutoachana huo siyo mwanzo wala mwisho wa sisi kuongea au kuwa pamoja,” alisema Shilole huku Barnaba akidakia.
“Mimi ni mwalimu wa muziki wa Shilole na ni mtunzi mzuri tu kwake so ukaribu wetu una maana nyingi.”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top