Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwili wa marehemu Musa Shija mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa mtaa wa Mwalugoye kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga aliyeuawa kwa kushambuliwa akiwa kwenye Fiesta usiku wa kuamkia leo katika uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza  mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema uchunguzi  wa kitaalam walioufanya unaonesha kuwa kijana huyo alipigwa na kitu butu kichwani na kusababisha kuvuja damu kichwani kutokana na kuvunjika kwa fuvu la kichwa.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mussa Athuman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa kijana huyo aliuawa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana nje ya fensi la uwanja mdogo wa Kambarage palipokuwa panafanyika tamasha la Fiesta.
Hata hivyo amesema jeshi la polisi litatoa taarifa kamili baadaye kwani linaendelea kufanya uchunguziHIVI NDIVYO ILIVYO KUWA NDANI YA  UWANJA MDOGO WA KAMBARAGE UMATI HUU WA WATU WAKISELEBUKA PASIKUJUA YAJAYO

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top