Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wananchi mjini Musoma wakiwa eneo la makaburi ya Musima Bus kushuhudia tukio hilo.
Eneo la makaburi ya Musima Bus walipozikwa baadhi ya marehemu wa ajali ya mabasi ya Mwanza Coach na J4 Express iliyotokea wiki iliyopita.
UMATI wa watu jana umejitokeza katika makaburi yaliyopo jirani na stendi ya Musa Mabasi, mjini Musoma baada ya kubaini kuwa kaburi mojawapo kati ya yale waliyozikwa marehemu wa ajali ya mabasi ya Mwanza Coach na J4 Express wiki iliyopita limefukuliwa na mwili wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Mzee Swai ukiwa nje na hauna baadhi ya viungo.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, mwili huo ulikuwa hauna baadhi ya viungo vya sehemu za siri kitendo kilichozua hasira kwa wananchi hao na kuwalazimu polisi kuingilia kati kuwatawanya.
Baada ya kuwatawanya wananchi hao, polisi walifanya uchunguzi kisha kushirikiana na baadhi ya wananchi hao kuuzika tena mwili wa mzee Swai huku wakiahidi kufanya uchunguzi zaidi.
  • Bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top