Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wananchi wakishuhudia lori la saruji lililopinduka na kuua dereva wake leo Septemba 09,2014, eneo la Milima ya Sekenke mkoani Singida.
Moja ya lori likitoa msaada wa kulivuta lori lililopata ajali kutoka bondeni.
Pichani juu na chini malori mengine ya mizigo yakipita karibu na eneo la tukio.
Dereva wa lori lililokuwa limebeba saruji kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza leo Septemba 09,2014, amefariki dunia baada ya lori hilo kupinduka eneo la Sekenke mkoani Singida.

Watu wengine wanne waliokuwa kwenye lori hilo wamejeruhiwa.

Mmoja wa mashuhuda wa ajai hiyo ameiambia tovuti hii kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kufeli breki kwa lori hilo lililokuwa likishuka Milima ya Sekenke na mpaka anaondoka eneo la ajali hiyo bado dereva (marehemu) na mmoja wa watu waliokuwemo aliyekuwa hai walikuwa bado wamenasa kwenye lori hilo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top