Manchester United wametoa dau la pauni milioni 55 kumtaka kiungo wa Real
Madrid Angel Di Maria, 26 (Daily Express), United pia watatazama
kumchukua kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, kutoka Barcelona
iwapo watashindwa kumpata Arturo Vidal, 27 (Daily Express), Borussia
Dortmund wamesema watafanya kila wawezalo kubaki na kiungo wao Marco
Reus, 25, licha ya mchezaji huyo kuwindwa na Arsenal, Liverpool na
Manchester United (Metro), Manchester City wapo
karibu kukamilisha usajili wa beki wa Porto Eliaquim Mangala, 23 kwa
kitita cha pauni milioni 32 (Daily Mail), beki wa kushoto wa Sevilla
Alberto Moreno, 22, atakamilisha uhamisho wake kwenda Liverpool wiki
ijayo, baada ya kucheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Real Madrid katika
michuano ya Uefa Super Cup, jijini Cardiff (Daily Mirror), Atletico
Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Roberto
Soldado, 29, kwa mkopo, lakini Spurs wangependa kumuuza kabisa (Daily
Telegraph), Tottenham wanamfuatilia winga kutoka Nigeria Moses Simon, 19
anayechezea Trencin (Daily Mirror), Everton wamekubaliana na Chelsea
kumchukua Christian Atsu, 22 kwa mkopo (Daily Mail), Real Madrid
wanajiandaa kutoa pauni milioni 10 kumchukua kipa, Petr Cech (Daily
Express), wakala wa winga wa Fiorentina Juan Cuadrado atasafiri kwenda
England weekend hii ili kuzungumza na Manchester United juu ya mkataba
wa pauni kati ya milioni 30 hadi 35 (Marca), Liverpool watamfuatilia
Ezequiel Lavezzi baada ya PSG kumwambia mshambuliaji huyo kuwa atauzwa
(Daily Express). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Weekend Njema! Na Salim kikeke
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment