Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Boss wa Manchester United Louis van Gaal anataka kumsajili kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, kwa mkataba wa pauni milioni 34 kiasi ambacho kitafikisha pauni milioni 200 za kununua wachezaji Old Trafford katika kipindi cha miaka miwili (Independent), United huenda wakamtoa Javier Hernandez, 26, kwenda Juventus, katika mkataba wa Vidal (Daily Express), Manchester United pia wanatarajia kutaka kumsajili Daley Blind, 24 kutoka Ajax kwa pauni milioni 18 katika siku chache zijazo (Sun), Arsenal wanaonekana kuzidiwa kete na Roma, kumsajili beki wa kati Kostas Manolas, 23 kutoka Olympiakos (Goal), Manchester United na Arsenal wamepata matumaini ya kuendelea kumfuatilia beki wa Roma Mehdi Benatia, 27, baada ya klabu hiyo ya Italia kuvunja mazungumzo na Bayern Munich (Daily Star), Arsenal huenda wakamfuatilia Danny Welbeck, 23, kutoka Man United, au Loic Remy, 27, kutoka QPR kuziba pengo la Olivier Giroud ambaye huenda akakosa kucheza kwa miezi mitatu kutokana na jeraha la kiwiko cha mguu (Daily Telegraph), Southampton wameanza kumfuatilia beki wa Atletico Madrid Toby Alderweireld, 25, na kuwazidi Monaco (Times), Tottenham wapo tayari kutoa pauni milioni 8 kumchukua nahodha wa Sevilla Federico Fazio, 27 (London Evening Standard) Chelsea wanazungumza na Roma kumchukua Mattia Destro, 23 (Daily Mirror), QPR wanakaribia kumsajili beki wa Liverpool Jack Robinson, 20 kwa mkataba wa pauni milioni 1 (Daily Mirror), West Ham wamemuulizia beki wa kati wa Bayer Leverkusen Philipp Wollscheid, 25, (Daily Mail), Sunderland, QPR na West Brom wanamtaka kiungo wa Leicester Andy King, 25, (Sun), AC Milan bado wanataka kumchukua Fernando Torres kutoka Chelsea, wakala wake akipendekeza kumchukua kwa mkopo, ingawa mshahara wake mkubwa unaonekana kuwa kikwazo (Metro), Napoli wataanza kumfuatilia tena kiungo wa Tottenham, Sandro kwa mkopo (The Times), Sporting wamewaambia Arsenal kuwa watakubali kitita cha euro milioni 30 kumsajili William Carvalho, kama Arsenal watakubali kumtoa Serge Gnabry, Francis Coquelin au Yaya Sanogo kwa mkopo (The Times), Everton wanakaribia kukamilisha usajili wa Samuel Eto'o. Roberto Martinez alikuwa akimtaka Danny Welbeck wa Man United, lakini alikatishwa tamaa na bei ya Pauni milioni 15 (The Times) na boss wa Inter Milan, Walter Mazzarri amewaambia watu wake kuwa wako huru kujaribu kumsajili Ezequiel Lavezzi kutoka Paris St-Germain (Tuttosport). Zimesalia siku sita kabla ya dirisha la usajili kufungwa. 
Bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top