Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mwili wa aliyekuwa msanii wa filamu Bongo, Patrick August, ‘Bryton’ ukiwa ndani ya gari.
TASNIA ya filamu Bongo imepata pigo tena baada ya msanii aliyekuwa akichipukia kwa kasi, Patrick August ‘Bryton’ kufariki dunia kwa ajali mbaya ya pikipiki.Akizungumza na paparazi wetu, Mwenyekiti wa Sherehe na Maafa kwa wasanii wa Wilaya ya Kinondoni, Masoud Kaftany alisema Bryton alipata ajali usiku wa kuamkia Jumapili maeneo ya Tabata - Relini wakati akirejea kwao maeneo ya Tabata - Kinyerezi.“Alikuwa akiendesha mwenyewe pikipiki, akavaana uso kwa uso na gari, ilikuwa ni ajali mbaya sana kwani marehemu alipasuka vibaya kichwa hali iliyosababisha damu nyingi kuvuja na kusababisha kifo chake,” alisema Kaftany.


Marehemu Patrick August, ‘Bryton’ enzi za uhai wake.
Baadhi ya sinema alizoigiza enzi za uhai wake ni pamoja na Muuza Genge na Mapenzi ya Fukara iliyomshirikisha Kulwa Kikumba ‘Dude’ na wasanii wengine. 


Mwili wa marehemu Bryton ulisafirishwa jana (Jumanne) kwenda  Rombo, mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yaliyotarajiwa kufanyikwa leo Jumatano.SHUKRANI KWA GPL
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
 

box;"> kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top