Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mtu mmoja amekufa papo hapo baada ya lori la kampuni ya kichina inayojenga barabara kuu ya Mbeya – Chunya kufeli breki zake likiwa kwenye mteremko mkali wa Isanga jijini Mbeya kisha kuparamia ukuta wa uzio wa nyumba ya makazi ya watu kabla ya kugonga nguzo ya umeme na kupinduka.
Ajali hiyo ambayo imetokea majira ya saa tatu asubuhi imehusisha lori la kampuni ya kichina inayojenga barabara kuu ya Mbeya – Chunya ambalo namba zake zimeng’olewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo punde tu baada ya ajali kutokea, lakini mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni breki za lori hilo kukatika likiwa kwenye mteremko mkali hali iliyosababisha kupoteza mwelekeo na kuingia kwenye makazi ya watu.
Wamiliki wa nyumba ambayo imeparamiwa na lori hilo, Emmanuel John Sangu na mkewe Monica Sangu wamesema kuwa kitendo cha lori hilo kuparamia nyumba yao kilihatarisha maisha yao na familia yao na kuwa ingawa wamenusurika wamepata hasara ya kuvunjiwa ukuta wa uzio wa nyumba yao.
Jeshi la polisi mkoani Mbeya limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa mtu aliyepoteza maisha alikuwa ni dereva wa lori hilo ambaye jina lake bado halijafahamika.
Chanzo ITV
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0712483331. 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top