Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Na Baraka Mpenja, 
RAIS mstaafu wa klabu bya Simba sc, ambaye ni mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage imelazwa Hospitali ya mkoa wa Dodoma baada ya kupata ajali ya gari akitokea Tabora kueleka mjini Dodoma leo.
Imeelezwa kuwa Rage alikuwa anakwenda Dodoma kuhudhuria vikao maalumu vya bunge la katiba.
Ajali hiyo imetokea eneo la Chigongwe mkoani Dodoma.



Imeripotiwa kuwa katika gari hilo, Mheshimiwa Rage alikuwa na abiria wengine ambao ni mbunge wa viti maalumu,  Munde Tambwe, Issa Chimwaga , Mwanahamisi Ramadhani na Dereva  John NKoya.
Abiria wote walipata majeruhi, isipokuwa dereva wa gari hilo, lakini wanaendelea kupata matibabu na hali zao zinakwenda vizuri.
Rage amezungumza akiwa wodini mkoani Dodoma, na kueleza kuwa amepata majeraha katika bega la mkono wa kushoto na eneo la nyuma ya mgongo.
Rage aliongeza kuwa ajali hiyo imetokea wakati dereva wa gari lao akijaribu kulipita roli, lakini ghafla dareva wa Roli hilo akaingia katikati ya barabara na ikamlazimu dereva wao kwenda pembeni ya barabara na gari kupinduka na kutumbukia kwenye korongo.


Mtandao huu unafuatilia taarifa kamili kuhusu ajali hiyo.
Ugua pole mwanamichezo Rage na abiria wengine wote.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
 kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top