kumbuka kwamba vyakula vyote vinaweza kuwa ni muhimu
mwilini lakini huzidiana kulingana na mahitaji na hali
ya mtu kwa wakati maalumu.
Mahitaji ya madini na vitamini mwilini wakati wa
ujauzito huwa ni makubwa, hususani madini ya kashiamu,
chuma na Vitamin B9 (folic acid).
MADINI YA KALISI (Calcium)
Wakati wa ujauzito, madini mengi ya kalisi husafirishwa
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa ajili ya kuimarisha
mifupa na meno. Katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo,
mama huhifadhi madini hayo mwilini mwake. Kiumbe
kinapokamilisha umbo lake katika kipindi cha miezi mitatu
ya mwisho, hifadhi hiyo huanza kutumiwa na kiumbe hicho,
hivyo mahitaji yake kuongezeka.
Katika kipindi hiki, mjamzito anatakiwa kula kwa wingi
vyakula vinavyoongeza madini ya kalisi kama vile maziwa
na vyakula vitokanavyo na maziwa. Kukiwa na upungufu wa
madini hayo, meno ya mama na mifupa huathirika pia.
MADINI YA CHUMA (Iron)
Mahitaji ya madini ya chuma nayo huwa makubwa kwa
wajawazito. Madini hayo ni muhimu kwa utengenezaji wa
damu ambayo huhitajika kwa wingi na mama pamoja na mtoto.
Madini joto hupatikana kwa kula kwa wingi vyakula kama
vile nyama, samaki, mayai, vyakula vilivyopikwa kwa
nafaka zisizokobolewa (ugali wa dona, mkate mweusi, n.k)
na mboga za majani kama vile spinachi na brokoli. Ili
kupata madini hayo ya kutosha kutokana na vyakula hivyo,
inashauriwa mjamzito kutumia pia vidonge vya Vitamin C
(Vitamin C food supplements).
VITAMIN B9 (Folic Acid)
Vitamini hii ni muhimu sana kwa mjamzito, ni kosa kubwa
sana la kiafya kwa mjamzito kuwa na upungufu wa vitamin
hii. Vitamin B9 ndiyo inayohusika na ukuzaji na uimarishaji
wa mfumo wa fahamu wa kiumbe tumboni.
Aidha, Vitamin hii ndiyo inayotoa kinga ili viungo vya mtoto
visiathirike na kuepusha uzaaji wa watoto walemavu au wenye
kasoro za viungo kama ‘midomo ya sungura’ na kadhalika.
Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin B9 ni pamoja na
mboga za majani, juisi ya machungwa, mapeasi, vyakula
vilivyopikwa kwa ngano na mchele (hasa brown rice) na mayai.
Hata hivyo, kutokana na hali ya vyakula vyetu, mjamzito
hawezi kupata kiwango kinachotakiwa cha vitamin hiyo kwa
kula vyakula peke yake.
Ili kupata kiwango cha vitamin hiyo kinachotakiwa, mjamzito
atatakiwa kutumia pamoja na vidonge vya lishe vya Vitamin
B9 ili kuepuka upungufu huo. Inashauriwa kutumia vidonge hivyo
miezi michache kabla ya kushika mimba na katika kipindi cha
miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito, kipindi ambacho vitamin
hiyo huhitajika kwa wingi.
Kwa ujumla, lishe bora ni muhimu kwa mjamzito katika kipindi
chote cha ujauzito wake. Matatizo mengi ya kuzaa watoto wenye
ulemavu wa aina mbalimbali, hutokana na upungufu wa madini na
vitamin muhimu mwilini katika kipindi cha ujauzito.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa Facebok fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
kama huja like ukurasa wetu wa Facebok fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment