Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


kaburi_afee5.jpg
Wananchi wakitolea kuchimba kaburi.
poa_b0878.jpg
Askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji Iringa wakijianda kuopoa mwili wa kijana kutoka mto Ruaha karibu na darajani eneo la Ipogoro, Manispaa ya Iringa.


gari_6f0a5.jpg
Gari la zimamoto likijiandaa kuondoka baada ya kumaliza kazi.
Na Friday Simbaya, Iringa
WAKAZI wa Manispaa ya Iringa walijitokeza kwa wingi katika mto Ruaha mdogo kushuhudia mwili wa kijana wa jinsia ya kiume ukiwa umeelea juu ya maji ya mto huo huku Jeshi la Zima moto na Uokoaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani hapa kuuopoa mwili ukiwa umeharibika vibaya.
Baada ya jeshi la uokozi kuopoa mwili huo waliuweka pembeni ya mto huo na kisha kuukabidhi kwa jeshi la polisi kwa ajili ya kuufanyia uchunguzi.
Kijana huyo ambaye hakufahamika kwa jina wala makazi yake alizikwa kandokando ya mto. huo baada ya kukosekana kwa ndugu zake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani iringa Ramadhani Mungi alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 10:00 Jioni eneo la ipogoro lililopo ndani ya manispaa ya iringa.
Kamanda mungi alisema kuwa mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa hauna nguo huku akibainisha kuwa marehemu anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 20 hadi 30.
Baada ya kuopolewa kwa mwili huo polisi kwa kuyshirikiana na jeshi la uokozi pamoja na vikosi vya ulinzi waliitisha mkutano wa utambuzi ili kama atajuikana aweze kuchukuliwa na ndugu zao lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza.
Hata hivyo polisi hao waliiamua kuzika mwili huo pembezoni mwa mto huo huku mwili huo ukiwa umeharibika vibaya.


"Ni kweli tulipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema na tulifika eneo la tukio na hatimaye kwa kushirikiana na jeshi la uokozi tulimuokoa japo kijana huyo hakuweza kufahamika jina wala kabila na sisi polisi hatuna taarifa yeyote ya mtu kupotea."alisema mungi
Wakati huo huo mashuhuda waliliambia MJENGWABLOG kuwa kitendo cha jeshi hilo kuzika mwili huo pembezoni mwa mto huo sio vizuri kutokana na mto huo kutumiwa na wakazi wengi wa manispaa ya iringa.
Mashuhuda hao ambao hawakupenda majina yao yaandikwe walisema kuwa jeshi hilo lisingetakiwa kuzika eneo hilo badala yake wangetafuta eneo lingine kwa ajili ya maziko licha ya mwili huo kuwa umeharibika.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
 kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top