MCHUMBA wa aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Maisha Plus (Season 2), Jack Dustan, Hamisi Ally ameibuka na kusema anamsaka mchumba wake huyo aliyepotea kwa takriban mwaka mzima tangu amvalishe pete ya uchumba.
Akizungumza na mwandishi wetu, Hamisi alisema kuwa alitarajia kuwa mpaka sasa wangekuwa wameshafunga ndoa lakini ghafla akasikia mchumba wake ametimka Bongo hivyo ndoto yake kuzimika.
Mchumba wa aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Maisha Plus, Jack Dustan, Hamisi Ally.
“Yaani kwa kweli nimeumia ndoto yangu kutoweza kukamilika toka mwaka jana, nampenda sana Jack na nilitamani awe mke wangu,nimesiki yupo China bora anirudishie pete yangu, la sivyo nitaendelea kumsaka hadi kieleweke,” alisema Hamisi.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyeza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment