
Wasiwasi: Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger alikiri kuwa kuna timu hatari katika droo ya UEFA iliyofanyika leo ijumaa.
ASERNAL watakabiliana na Besiktas katika mchezo wa raundi ya pili ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA).
Arsene
Wenger alikwepa kukutana na Athletic Bilbao, Lille , FC Copenhagen,
Standard Liege, lakini sasa atachuana na timu hiyo ya Uturuki ambayo
siku za karibuni ilimsajili Demba Ba kutoka Chelsea kwa ada ya uhamisho
ya paundi milioni 4.7.
Besiktas
ilimaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita, lakini imefuzu kucheza
UEFA baada mabingwa Fenerbahce kufungiwa kucheza mechi za michuano ya
ulaya kwa kosa la kupanga matokeo ya mechi ya nyumbani.

Arsenal atacheza michuano ya ulaya kwa mwaka wa 17 mfululizo
Amefungiwa: Beki Bartosz Bereszynski alitolewa dakika za mwisho katika kipigo cha Celtic

Wachezaji wa Legia Warsaw wakishangilia baada ya dakika tisini, huku Stefan Johansen akiacha hoi.
Arsenal
watasafiri kwenda Uturuki kucheza mechi ya kwanza Agosti 19 au 20 mwaka
huu na mechi ya marudiano itapigwa Emirates Agosti 26 au 27.
Kiungo
wa Asernal mwenye asili ya Uturuki, Mesut Ozil alifurahishwa na droo na
kuandika kwenye mtandao wa Twita akisema: 'Droo nzuri! tayari
tunaangalia mbele kuelekea mechi dhidi! @Besiktas! #Turkey #İstanbul
#Arsenal #AFC #UCLdraw'.
Wakati
huo huo, leo asubuhi, Celtic wamepewa nafasi ya kusonga mbele baada ya
kubainika kuwa klabu ya Legia Warsaw ilimchezesha mchezaji asiyekuwa na
vigezo.
Kamati
ya nidhamu ya UEFA ilikutana na kutoa maamuzi kabla ya droo mjini Nyoni
na kuamua kuwa Celtic wanatakiwa kupewa ushindi wa mabao 3-0 katika
mchezo wa pili na inamaanisha wamesonga mbele kwa magoli ya ugenini.
DRAW NZIMA HII HAPA
FULL CHAMPIONS LEAGUE PLAY-OFF ROUND DRAW
Maribor vs Celtic
Red Bull Salzburg vs Malmo
Aalborg vs APOEL
Steaua Bucharest vs Ludogoret
Slovan Bratislava vs BATE
Besiktas vs Arsenal
Standard Liege vs Zenit
Copenhagen vs Bayer Leverkusen
Lille vs Porto
Napoli vs Athletic Bilbao
Ties to be played on the 19/20 and 26/27 August
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment