Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mgogoro umeibuka nchini India baada ya polisi mwanamke nchini humo kucheza densi ukumbini na muigizaji maarufu Shah Rukh Khan katika tamasha la polisi lililofanyika katika jimbo la Bengal Magharibi.

Wanasiasa wa upinzani wamekosoa densi hiyo, wakisema afisa huyo wa polisi kucheza densi akiwa avelia sare zake, imehujumu heshima kwa polisi.
Kiongozi wa jimbo la West Bengal,Mamata Banerjee, aliyehudhuria tamasha hilo, pia alishambuliwa kwa kuruhusu tamasha hilo kufanyika.
Polisi huyo mwanamke na muigizaji Shah Rukh Khan bado hawajatoa tamko lolote kuhusu sakata hiyo.
Densi hiyo, ilifanyika katika tamasha maalum la polisi lililofanyika siku ya Jumamosi.
Shah Rukh Khan ni mmoja wa waigizaji mashuhuri nchini India na duniani , na hivi maajuzi alitajwa kama balozi wa jimbo la Bengal Magharibi.
Rais wa chama cha upinzani cha Congress katika jimbo hilo, Adhir Ranjan Chowdhury alituhumu mkuu wa jimbo hilo Bi Banerjee kwa kukiuka, katiba kwa kumruhusu afisaa hiyo kucheza densi akiwa amevalia sare yake.


katiba hairuhusu mtu kucheza densi akiwa amevalia sare za kazi. Ni aibu tupu kwamba sifa ya idara ya polisi ilivunjiwa heshima hivyo. Kwa kuruhusu afisa wa polisi kucheza katika hali ile, alivunja katiba ya India
alinukuliwa akisema afisa mkuu wa upinzani jimboni humo.
Taarifa zinasema kuwa kamishna mkuu wa zamani wa polisi Nirupam Som alisema,
wakati wa muhula wangu uongozini, singeruhusu hata kidogo polisi kucheza densi kama vile
Lakini baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii, walipuuza sakata hii iliyozua mgogoro huu wote kama kutokuwa kichekesho.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0712483331.
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top