Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This




Ndugu wa marehemu Suzana Adamu wakilia kwa uchungu.

BINTI mmoja aliyefahamika  kwa  jina la Suzana Adamu (20), mkazi  wa Mazizini- Ukonga jijini Dar amefariki dunia kwa kugongwa na gari akitoka  kukamilisha taratibu za  viza kwa ajili ya kwenda  Dubai kufanya kazi.Kwa mujibu wa  mashuhuda  wa ajali  hiyo, ilitokea Agosti Mosi, mwaka huu saa 2:30  usiku katika Mtaa wa Mahita ambapo mrembo huyo alikuwa akitoka mjini kwa  ajili ‘shoping’ pia  kuaga ndugu na jamaa ili kesho yake apande ndege kwenda Dubai ambako alipata kazi ya mkataba wa miaka miwili.
Ndugu na jamaa wakiomboleza msiba huo.
Ilidaiwa kuwa, akiwa anarudi nyumbani kwao, alipofika eneo hilo alizolewa na gari lililokuwa limekodiwa  na watu waliokuwa wanatoka  ufukweni kula Sikukuu ya Idd.

Mashuhuda walisema dereva wa gari hilo alikuwa  mwendo kasi na hivyo kumvaa binti huyo aliyekuwa akitembea kwa miguu.Imeelezwa kuwa, kutokana na mwendo kasi, baada ya kumgonga Suzana gari hilo lilikwenda  kugonga ukuta.Mwili wa marehemu ukishushwa kwenye gari nyumbani kwao.
Akizungumza na Amani kwenye msiba wa binti yake, baba mzazi wa mrembo huyo, Adamu Mohamed alisema siku ya maziko ya marehemu huyo ndiyo ilikuwa safari yake ya kwenda Dubai.
“Ndugu mwandishi, kaburini ndiyo Dubai ya mwanangu. Sasa si mkataba tena wa miaka miwili bali amepata mkataba wa kudumu huko alikokwenda,” alisema mzee huyo kwa masikitiko.

Marehemu Susan Adamu enzi za uhai wake.
Alisema Suzana ni mtoto wake wa nne kuzaliwa, amemuacha katika  wakati mgumu kwa sababu alikuwa   tegemeo kubwa ndani ya familia. Marehemu Suzana alizikwa Agosti 2, mwaka huu katika Makaburi ya Kijiji cha Mfuru, Kata ya Maneremango, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Mmoja wa marafiki wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha, alisema kifo cha Suzana ni pigo kubwa kwao kwani alikuwa mkarimu aliyependa kuwasaidia wenzake.
>>>>>Credit GPL

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa   

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top