Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Boss wa Manchester City Manuel Pellegrini anapanga kumchukua Didier Drogba, 36, ambaye pia anasakwa na klabu yake ya zamani Chelsea (Daily Star), meneja wa Manchester United Louis van Gaal anataka kutoa pauni milioni 17 kumchukua beki mkabaji wa Ajax Daley Blind, 24 (Daily Express), United pia wameripotiwa kuwa karibu kumsajili beki wa kati wa Borussia Dortmund Mats Hummels, 25, kwa pauni milioni 16 (Daily Mail), Tottenham wameambiwa watoe pauni milioni 25 kama wanamtaka kiungo wa Real Sociedad Antoine Griezmann, 23, ambaye pia anafuatiliwa na Chelsea na Monaco (Daily Telegraph), boss wa Arsenal, Arsene Wenger amesema hatosajili mshambuliaji msimu huu na hivyo kufuta tetesi zinazomhusisha na Mario Balotelli wa AC Milan (Daily Mirror), kiungo wa Ureno Thiago Mendes, 23, ametupilia mbali uwezekano wa kurejea Chelsea na angependa kusalia Atletico Madrid miaka miaka mingine miwili (Daily Express), PSG watakwepa sheria za Fifa za fedha kwa kumchukua Angel Di Maria, kwa mkopo kwa mwaka mmoja kutoka Real Madrid. Di Maria anasakwa pia na Man United (Daily Express), Arsenal, Chelsea na Man United wanamtaka beki Reece Oxford, 15, baada ya kinda huyo kuonesha kipaji msimu uliopita akiwa na West Ham ya vijana (Daily Star), Arsene Wenger atamruhusu Thomas Vermaelen kwenda Manchester United, ikiwa tu atarhusiwa kumchukua Phil Jones au Chris Smalling (Daily Mirror), Chelsea watampa Didier Drogba mkataba wa miezi 12 wa kucheza ambao hautakuwa na kipengele cha kuwa kocha, ingawa Chelsea wapo tayari kuzungumzia hilo (Daily Telegraph), mshambuliaji wa Lille Divock Origi anakwenda Boston Marekani kuungana na Liverpool ambao wapo katika ziara ya mechi za kabla ya msimu. Atafanyika vipimo kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 10. Huenda pia akarejeshwa Lille kwa mkopo (Daily Star). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. 

Tetesi hizi kwa hisani ya Salim Kikeke-- Cheers!!

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top