Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
West Ham wanataka kumsajili mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto'o, 33 ambaye aliondoka Chelsea msimu uliopita (Sun on Sunday), Inter Milan wanafikiria kumtoa Fredy Guarin, 28, kubadilishana na Javier Hernandez, 26, kutoka Manchester United (Sun on Sunday), Romelu Lukaku aliyecheza Everton kwa mkopo msimu uliopita, anataka uhamisho wa kudumu kwenda Goodison Park (Talksport), Arsenal wanakaribia kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Shakhtar Donetsk, Douglas Costa, 23 ambaye ameomba kuondoka Ukraine kwa sababu za matatizo ya kisiasa nchini humo (Caughtoffside), Atlètico Madrid wamefikia makubaliano ya kumsajili Antoine Griezmann, 23 kutoka Real Sociedad kwa pauni milioni 24 (AS), meneja wa. Manchester United bado ana nia ya kumsajili kiungo wa Roma Kevin Strootman, 24, licha ya mchezaji huyo kuwa majeruhi kutokana na kuumia goti (Sky Sports), Real Madrid wanapanga kumchukua Radamel Falcao, 28, kwa mkopo na uhamisho wa kudumu mwaka 2015 (AS), jaribio la Stoke City kumsajili Oussama Assaidi, 25, kutoka Liverpool kwa pauni milioni 7, huenda likashindikana kutokana na winga huyo kutaka mshahara mkubwa (Daily Express), mshambuliaji wa Lille Divock Origi, 19, anakaribia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 12.5 kwenda Liverpool (Sunday Mirror), Sami Khedira anataka mshahara wa pauni milioni 7.1 kwa mwaka ili kujiunga na Arsenal (La Sexta), Arsenal wanafikiria kupanda dau kumchukua kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin (Daily Star), Angel Di Maria anajiandaa kusaini mkataba wa miaka mitano siku chache zijazo na Paris St-Germain (Marca). 
Na salim kikeke
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
 
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top