Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo (Jumatano) asubuhi.
Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako darasani.
Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea. Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kilifika wakati tayari mabweni hayo yameshateketea.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli yaliyoteketea kwa moto, akiongozana na mkuu wa shule hiyo mwalimu Agnes Nyange.na jiachie blog
Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh Edward Lowassa  ametembelea shule hiyo na kuahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati  utaratibu unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida.
Gharama za kuwasafirisha wanafunzi hao ni shilingi laki Saba. Aidha Mh Lowassa amesema kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.
Kikosi Cha zimamoto kikijaribu kupambana na moto ulioteketeza mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo Monduli mjini yaliyoteketezwa kwa moto.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa afisa elimu wa Monduli mwalimu Shaaban Mgunya wakati alipotembelea mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli yaliyoteketea kwa moto.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top