Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MAUSTADH jijini Dar es Salaam wamefikia uamuzi mzito wa kutembeza bakora kwenye vijiwe korofi vya warembo wanaojishughulisha na biashara haramu ya kuuza miili almaarufu kama machangudoa au machangu kwa kile kilichodaiwa kuwa wanasafisha jiji kutokana na kero za vishawishi vya kuharibiwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Maustadh wakimuadhibu mmoja wa machangudoa hao.

Kwa mujibu wa sosi aliyewasiliana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, maustadh hao walianza oparesheni yao waliyoibatiza jina la ‘Safisha Jiji’ maeneo ya Sinza kwenye mitaa ya Shule ya Msingi ya  Mapambano na jirani na msikiti uliopo maeneo ya Afrika Sana.
Wakati maustadh hao wakiwafungia kazi na kutembeza bakora, OFM ilifika maeneo
hayo na kufanikiwa kunasa tukio zima ambapo iliwashuhudia warembo hao waliokuwa wakijiuza kwa madai ya kusaka fedha za sikukuu, wakipewa kibano cha kutosha.
Mmoja wa machangudoa hao akidhibitiwa.
Wakizungumza na OFM baada ya sakata hilo, maustadh hao walisema wamechoshwa na uchafu unaofanyika kwenye makazi yao huku wakifunguka kuwa mara kadhaa wanaporudi nyumbani wakitokea msikitini, machangu hao huwang’ang’ania wakiwashawishi kufanya nao ngono bila kujua wapo katika mfungo.
“Tumechoshwa na ufuska, mbaya zaidi hawa machangu wanafikia hatua ya kutung’ang’ania wakitulazimisha tuwanunue bila kujali kama tunatoka msikitini kuswali,” alisema mmoja wa maustadh hao na kuongeza kuwa wanauheshimu mwezi huu mtukufu ndiyo maana wameamua kutembeza bakora kwa machangu hao.
Warembo hao walishuhudiwa wakiwaomba msamaha maustadh hao na kudai kuwa wamekoma, hawatarudia tena kuwasumbua maustadh.“Jamani kaka zangu nawaomba msinichape sana nina ujauzito, naomba mnichape kwenye makalio nimekoma sitarudia tena,” alisema mmoja wa machangudoa aliyekuwa akitembezewa kichapo.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
 
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top