Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
USIPIME! Habari ya mjini kwa sasa ni uzinduzi wa nyimbo mbili za Ally Saleh ‘Ali Kiba’, Mwana na Kimasomaso ambazo atazizindua kwenye Tamasha la Matumaini Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mkali wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’
Kiba ambaye ni mkongwe kunako muziki wa Bongo Fleva, amefunguka yeye siku zote ni staa na huwa hakosei hivyo mashabiki watarajie burudani kali siku hiyo.
Kiba ameizungumzia shoo yake katika tamasha hilo kwamba itakuwa spesho hivyo mashabiki wategemee mambo yafuatayo;

Shoo kali
Katika shoo zake zote huwa habahatishi.
Amekuwa ni msanii wa kwanza kutoka Bongo kwa kupiga idadi ya shoo nyingi nje ya nchi kuliko msanii yeyote hata katika matamasha ya ndani ya Bongo amekuwa akiteka hisia nyingi za mashabiki, kwenye Tamasha la Matumaini amesema itakuwa ni zaidi ya burudani.

‘Ali Kiba’ akipozi.
Kuchomoka kivingine
Baada ya kukaa kimya kwa muda sasa mfalme huyo mwenye sauti ya ajabu, sauti ya kumfanya kila shabiki aikumbuke inapopotea kidogo, amesema anakuja kivingine ambapo atapiga muziki wake kwa mpangilio maalum kuanzia sauti nzuri ya kuwabembeleza.

Habakishi kitu
Kiba amesema siku hiyo hatabakisha kitu, atazipiga nyimbo zote kali kuanzia zile za zamani kama Single Boy, Dushelele, Mac Muga, Run Dunia na nyingine kibao bila kusahau Mwana na Kimasomaso ambazo ndiyo habari ya mjini.

Tamasha hilo linatarajiwa kupambwa na matukio kibao ya kusisimua kama ngumi za wabunge, mechi za mpira wa miguu za wabunge na wasanii wa Bongo Fleva, Bongo Movie bila kusahau burudani nzuri kutoka kwa wasanii wanaotamba katika muziki wa Injili.
Burudani zote hizo kwa pamoja, mashabiki watazishuhudia kwa mtonyo wa shilingi elfu tano tu huku sehemu ya mapato yatakayopatikana ikipelekwa katika mfuko wa elimu nchini.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top