Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Watu watatu wakazi wa Mwananyamala Jijini Dar Es Salaam wamejeruhiwa katika tukio lililohusisha risasi za moto linalodaiwa kufanywa na polisi baada ya kukutwa wakikesha kwenye ngoma maarufu za Kigodoro, ambazo tayari zimekwishapigwa marufuku na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi na nusu jioni katika eneo la shule ya msingi kisiwani ambapo mmoja  wa  majeruhi hao  tayari amekwisahruhusiwa kurudi nyumbani na mwingine akiendelea na matibabu kwenye hospitali ya Mwananyamala.
 

Wakiwa kwenye ngoma hiyo maarufu Jijini Dar es Salaam ya Kigodoro, eneo la Kisiwani mwananyamala, mara gahfala polisi walivamia eneo hilo, na kusimamisha shughuli nzima kwa madai ya kucheza wakiwa hawana nguo, jambo ambalo ni kinyume na maadili.
  
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni Kamishna msaidizi Camillius Wambura anathibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top