Yusta Lucas akionyesha majeraha ya meno aliyong'atwa na bosi yake.
NYUMAya pazia! Yule msichana Yusta Lucas (20) mwenyeji wa Mkoa wa Tabora ambaye alifika jijini Dar kufanya kazi ya u-hausigeli na kufanyiwa ukatili wa kutisha na bosi wake kisha habari zake kuandikwa, ametoa siri nzito, Uwazi limemegewa.
Akizungumza
kwa uchungu na gazeti hili akiwa wodini kwenye Hospitali ya Mkoa wa
Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala jijini Dar, Yusta ambaye amefanya kazi
kwa tajiri yake huyo kwa miaka mitatu alisema:
“Kwanza nataka watu wajue kuwa mwajiri
wangu ni binamu yangu, alinileta hapa Dar kwa ajili ya kumsaidia kazi
za ndani pamoja na kumlelea mwanaye.
“Kipigo hasa kilianza mwanzoni mwa mwaka
huu ikiwa ni pamoja na kuning’ata kwa meno mwili mzima, ndiyo maana
mwili wangu wote unaonekana una mabakamabaka.
“Mateso yangu majirani walikuwa wakiyajua
kutokana na kilio changu lakini walikuwa wanashindwa kunisaidia kwa
sababu ya ushirikiano mdogo.
“Kwanza nashangaa sana kwa adhabu yake ya
kuning’ata meno mpaka damu zinabaki kwake. Je, kama nina virusi vya
Ukimwi si na yeye anavipata?
“Sijajua alikuwa anapata wapi ujasiri wa
kuning’ata meno. Kwa kweli nimeteseka kwa muda mrefu sana. Mungu ndiye
anajua, lakini nawashukuru sana majirani walioliona hilo na kuamua
kuchukua hatua.”
Yusta Lucas akiwa wodini kwenye Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala jijini Dar.
KUHUSU MAISHA YA TAJIRI WAKE
Aidha, Yusta alianika mienendo mitano ya bosi wake huyo na kusema imekuwa ikimshangaza sana.
MWENENDO WA KWANZA
“Mimi katika kuishi kwangu pale sijawahi
kumwona jirani yeyote amekuja ndani kusalimia wala yeye kwenda kwa
jirani kufanya hivyo jambo ambalo si la kawaida.”
MWENENDO WA PILI
“Yeye (bosi wake) hana mume. Lakini tangu
nimeishi pale kwa miaka mitatu sijawahi kumwona mwanaume ameingia ndani
ya nyumba achilia mbali wanawake wenzake, hata mgeni. Kifupi yeye ni
yeye kwa pale nyumbani kama ana marafiki labda wanakutana mbali.”
MWENENDO WA TATU
“Muda wake wa kurudi nyumbani siku
zote ni usiku mnene, amewahi sana ni saa mbili usiku. Kwa hiyo, muda
mwingi mimi ndiyo huwa nyumbani.”
MWENENDO WA NNE
“Anajiweza, sijui kwa nini aliamua
kunifanyia hivi. Maana mtu ana gari, anaendesha mwenyewe na anasema ana
hela, ndiyo maana namshangaa kuniadhibu kwa kuning’ata kwa meno.”
MWENENDO WA TANO
“Sikumbuki lini nimewahi kumwona akicheka. Muda mwingi anaonekana amekasirika tu kiasi kwamba nimekuwa nikimwogopa siku zote.”
OMBI KWA SERIKALI
Yusta alisema kufuatia matatizo makubwa yaliyompata ameiomba serikali imsaidie aweze kurudi nyumbani kwao Tabora.
SHUKURANI KWA MAJIRANI
Yusta alitoa shukurani kwa majirani waliojitokeza kuokoa maisha yake ambapo alisema kama wasingekuwa wao hajui ingekuwaje.
MANENO YA MUUGUZI
Kwa upande wa hospitali hiyo,
muuguzi kiongozi wa zamu siku hiyo, Mahija Swalehe alikemea tabia za
waajiri wa wafanyakazi wa ndani kuwatesa na kuiomba serikali kuliangalia
suala hilo kwa jicho la tatu ili kukomesha vitendo hivyo.
TUJIKUMBUSHE
Yusta alikumbwa na masaibu hayo kwa
muda mrefu hadi hivi karibuni majirani wakiwa na polisi walipovamia
nyumba hiyo na kumkamata bosi wake kisha kumpeleka Kituo cha Polisi cha
Oysteraby, Dar ambako anashikiliwa na yeye kupelekwa Hospitali ya
Mwananyamala kwa matibu baada ya kukutwa na majeraha.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa
Kinondoni, ACP Camillius Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kusema mtuhumiwa ametiwa mbaroni.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment