Baada
ya kukatika kwa umeme majira ya saa moja na dakika shirini na tatu na
kusababisha karibu mikoa yote ambayo imeunganishwa na Gridi ya taifa
kukosa nishati ya umeme na kusimamisha shughuli za bunge ikiwemo zoezi
la upigaji wa kura ya bajeti ya serikali,
mkurugenzi mtendaji wa shirika
la umeme nchini Tanesco mhandisi Felchesim Mramba ametoa afafanuzi juu
ya kukatika huko kwa umeme na kubainisha kuwa mafundi wa shirika hilo
wanaendelea kufanya uchunguzi nini kimesababisha tatizo la kukatika kwa
umeme na kusababisha usumbufu kwa wateja wa Tanesco.
Amesema
hali hiyo imetokana na kuzimika ghafla kwa mitambo na kusababisha nchi
nzima kuwa gizani,ambapo chanzo cha kuzimika kwa mitambo hiyo bado
hakujajuliana.
Amesema kikubwa kinachofanyika sasa ni kurejesha huduma wakati uchunguzi ukiendelea kufanyika
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment