Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Professor-Jay1-copy-800x596Msanii mkongwe wa Hip Hop Proffesor Jay amesema kuwa kushindwa kwa Diamond kuchukuwa tuzo za MTV kusimvunje moyo kwakuwa alikuwa anashindana na wasanii wakubwa sana Africa.

Akizungumza na bongo5 leo ,Proffesor Jay amesema kuwa nafasi aliyopata Diamond na kushindana na wasanii hayo ni ushindi mkubwa wake.

Diamond lazima ajue katika mashindano kuna kushinda na kushindwa, Kitu ambacho ninaweza kumwambia Diamond asikate tamaa, ameshindanishwa na wasanii wakubwa sana ambao pia ni advantage kwake ,msanii kama Davido pamoja na kufanya muziki mzuri tutambue kuwa nyuma yake kuna Wanageria zaidi ya milioni 150, ambao kiukweli wenzetu wameamka sana kuchangia kuwa support wasanii wao, 

sisi Watanzania tumekuwa tunazungumza kwa maneno mengi kulipo vitendo ,so mtu kama Davido ameshinda kwa kupigiwa kura na watu wake wengi na muziki wake umefika afrika nzima . Kwaiyo kushindwa kwake Diamond asichukulie kukata tamaa ,yeye achukulie kama changamoto na kuwashawishi Watanzania na mashabiki wake kuendelea ku support muziki wake ili afike mbali zaidi ,

 naamini kuna kila dalili kwa Diamond kuendelea kufanya vizuri zaidi hapo mbeleni, pia nataka niwaambie Watanzania kwamba mtu anapoiwakilisha Tanzania tujitaidi kuweka tofauti zetu nyuma na kum,support wasanii wetu kwa sababu ushindi wake ni mafanikio makubwa ya muziki wetu,wasanii na wetu, na taifa kwa ujumla” Alisema Proffesor Jay.


Katika hatua nyingine Proffesor Jay amesema kuwa kesho anaingia mzigoni kuanza kushoot video ya ‘Kipi Sijasikia’
“Kesho naanza ku,shoot video ya Kipi Sijasikia, kilichotokea nilikuwa namsubiri tu Diamond, kwa sababu ratiba yake ilikuwa imebana sana, kila kitu sasa hivi kipo set, na tunafanya na Adam Juma, kilichotufanya tu delay kidogo ni kwa sababu alikuwa ameagiza Red na vitu vingine, kwaiyo vikawa vimechelewa kidogo lakini baada ya kuingia vyombo vyake, kesho tunaanza lakini ataujajua tutamaliza lini. 

Adam amenivutia sana sasa hivi kwa sababu ya kubadilisha kamera , Adam ana skills kubwa ya kutumia kamera , lakini kamera ambazo alikuwa akitumia mwanzo zilikuwa zinambana kidogo lakini sasa hivi kwa kuleta kamera hiyo Red na vitu vingine kama hivyo tunategemea uwezo wake anaweza akaonyesha kwa mapana zaidi , na pia tumejaribu tunatumia advantage ya Diamond huko anakozunguka kujaribu kufanya connection, kwa sababu Diamond anaweza kusaidia muziki wetu kifika mbali zaidi”Alisema Proffesor.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top