Twende kazi mwana: Neymar (kushoto) na Dani Alves wamebadili mtindo wa nywele zao.
NYOTA wa Brazil, Neymar sio `mchawi` inapofika wakati wa mitindo ya nywele .
Baada
ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa ufunguzi wa kombe la dunia
dhidi ya Croatia, Neymar ameonesha mtindo mpya ya nywele zake kwenye
mazoezi ya kikosi cha Brazil leo asubuhi. Naye beki wa kulia, Dani Alves
anayeichezea Barcelona amebadilisha mtindo wa nywele zake.
Neymar
amenyoa nywele za pembeni, huku akiziacha za juu na kuzichania kwa kwa
mbele. Naye Alves amezikata na kuziweka fupi fupi.
Neymar ndiye alifunga mabao 2 katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Croatia
Mashabiki wa Brazil wakimtazama shujaa wao na mtindo wake mpya wa nywele.
Neymar amekuwa akibadilisha mara kwa mara mtindo wa nywele zake wakati wa mashindano.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment