Wewe unadhani
ukatili wa kijinsia ni kwa wazazi au walezi tu kwenda kwa watoto?
Hapana hata kwa baadhi ya wazazi pia inatokea kwa kufanyiwa ukatili na
watoto wao ila hushindwa kujitokeza hadharani kusema mbele ya jamii kwa
aibu au kufanya hivyo mara chache.Hii imemtokea mwanamke huyu aitwaye
Bobbi kutoka Southampton , Uingereza ambapo anasimulia jinsi
alivyofanyiwa ukatili na mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa akitaka
kumchoma kisu na wakati mwingine kumvizia akitaka kumuua.
Mtoto
huyo aitwaye JJ mara kadhaa amekuwa akifanya mashambulizi ya vurugu kwa
mama yake kwa kumpiga, kumrushia vitu kichwani na wakati mwingine
kumvuta nywele ambapo katika tukio jingine alijaribu kumchoma kisu
akitaka kumuua.
Hali hiyo
ilimlazimu Bobbi kuondoa vitu vyote vyenye ncha kali karibu na nyumbani
ili kuepusha hatari ambapo hata kwa baba yake wa kambo imekuwa ngumu
kwake kuishi pamoja na mtoto huyo kwani ni vita kali.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment