Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetelekezwa na mama yake.
VITUKO uswahilini! Mtoto wa mwenye umri umri wa mwaka mmoja ambaye jina halikufahamika ameokolewa na Oparesheni Fichua Maovu ya Global Publishers baada ya kudaiwa kutelekezwa kwa siku nzima na mama yake mzazi, Mama Sofia.
Tukio
hilo la aina yake lilijiri Juni wikiendi iliyopita maeneo ya
Somanga-Magomeni, Dar ambapo kwa mujibu wa wasamaria wema waliomuona
mtoto huyo, alionekana majira ya asubuhi akirandaranda barabarani.
Walisema walidhani alikuwa akielekea nyumbani kwao lakini hadi jioni walishangaa kumuona bado anarandaranda mitaani mwenyewe.
Mtoto huyo akiwa na msamaria.
Baadaye
OFM ilipewa taarifa na kufika eneo la tukio ambapo ilipata maelezo kuwa
mama wa mtoto huyo huwa na tabia ya kumwacha mwanaye mara kwa mara
mtaani bila kumjali.
OFM
ilifikisha suala hilo kwa mjumbe wa mtaa huo ambaye alimtambua mtoto
huyo mara moja kwa kuwa alikuwa akiishi naye nyumba moja hivyo
alimpeleka kwa wazazi wake huku akiwapa onyo kali.
GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment