Njaa
mbaya! Kama ulikuwa unadhani ile Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global
Publishers imenywea, basi umenoa! Safari hii imenasa tukio la mrembo
akijihusisha na biashara haramu ya ngono nje ya ofisi za serikali
Tukio hilo lisilo la kimaadili lilijiri usiku wa manane wikiendi iliyopita kwenye ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama, Dar.
Baada
ya kupokea kero kwa wakazi wazalendo wa eneo hilo kuwa ofisi yao
inanajisiwa, OFM ilifanya uchunguzi wake wa kina na ilipojiridhisha
ndipo ikaweka mtego.
Kabla ya tukio ilisemekana kuwa pamoja na
ngono kufanyika waziwazi na machangudoa waliopo maeneo mbalimbali ya
Sinza na Kijitonyama, Dar, siku hizi wadada hao wafikia hatua mbaya
zaidi kwa kufanyia maeneo yenye hadhi na sifa maalum kama viwanja vya
shule za msingi, nje ya ofisi za watu, karibu na misikiti na makanisani.
“Yaani
siku hizi hawa wasichana hawani soni hata tone, wamefikia hatua ya
kufanyia ngono sehemu rasmi tena bila kificho, kwa mfano pale maeneo ya
Sinza-Mapambano si wanafanyia ngono kwenye uzio wa shule!
Ukifika pale asubuhi utakuta kondomu kibao. Hata pale kwenye ofisi za mtendaji utawaona wanafanyia ngono kule nyuma kwenye miti bila hata ya hofu,” alisema mmoja wa wakazi wa Kijitonyama.
Tukirudi kwenye tukio, OFM ikiwa doria
chimbo, mishale ya saa nane na nusu usiku, hakukuwa na purukushani
yoyote iliyoonesha viashirio vya ngono nje ya ofisi hiyo
Ghafla
nusu saa baadaye makamanda wa OFM waliokuwa katika kufunga vifaa vyao
vya kazi, walishuhudia Bajaj ikisimama mbele na kumshusha mrembo mmoja
maarufu kwa jina la Shishi akiwa na ‘mteja’ kisha wakajibanza kwenye
miti nje ya ofisi hiyo.
Makamanda
wa OFM walikuwa makini kufuatilia mchezo mzima ambapo waliwashuhudia
wawili hao wakitandika khanga tayari kwa ajili ya ‘mambo yao’.
Baada ya kila kitu kuwa sawa ndipo
makamanda walipiga simu kwa askari wa doria waliokuwa maeneo hayo na
kuwavamia kisha kuwatia nguvuni ambapo katika kujitetea mrembo huyo
alisema kuwa, mteja wake alimlazimisha kufanyia ngono katika eneo hilo
kwa sababu alimaliza fedha zote kwa kumnunua yeye pombe.
“Najua
eneo hili ni la serikali lakini huyu jamaa alikuwa na fedha kidogo na
nyingine ya gesti nikaamua bora yote anipe mimi kisha nikamleta hapa.
Nisameheni sitarudia,” alisema mrembo huyo huku mteja wake aliyeonekana
kukolea kinywaji akiomba aachiwe kwa kuwa hakujua alilokuwa akilifanya.
Hadi OFM inaondoka eneo la tukio wawili hao
walikuwa wametaitiwa mikononi mwa polisi ambapo kwa kawaida kisheria
watashitaki kwa kosa la uzembe na uzururaji.
Alipotafutwa
Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama ili kuzungumzia ishu hiyo hakupatikana
hewani na hata alipofuatwa ofisini kwake kulikuwa na kufuli kubwa.
Imeandaliwa na Chande Abdallah, Richard Bukos, Deogratius Mongela na Issa Mnally.
>>>GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment