Mauaji hayo
ya kinyama yamefanyika saa saba usiku wa kuamkia june 28,2014,baada ya majambazi
hayo kuvunja milango ya nyumba aliyokuwa amelala kiongozi huyo na
familia yake katika kijiji cha Kwikuba kabla ya kumshambulia kwa bapa za
panga mke wamarehemu Bi Agness Wambura ambaye alilazimika
kuwapa kiasi cha shilingi laki nne ambazo alizikopa kutoka
katika taasisi moja ya fedha.
Afisa
upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Mara Acp Rogati Mlashan,akizungumza
na ITV akiwa eneo la tukio, amesema baada ya majambazi hayo kuvunja
milango miwili ya nyumba hiyo, walipiga risasi tatu na moja kumpata
kichwani kiongozi huyo wa CCM na kufariki dunia papo hapo na
kusema kuwa jeshi la polisi litafanya kila liwezavyo ili
kuhakikisha wote walihusika kufanya uhalifu huo wanakamatwa na kufikishwa
katika vyombo vya sheria.
Kwa upande
wao baadhi ya viongozi serikali katika kata ya
Busambala,wakizungumzia tukio hilo pamoja na kuonyesha masikitiko yao
baada ya
kupata taarifa za kifo cha kiongozi huyo wa CCM,wameliomba jeshi la
polisi
kuendesha msako mkali ambao utawesha kukamatwa kwa wahusika,hatua
ambayo wamesema itasaidia kuondolea wananchi hofu kubwa waliyonayo
sasa.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment