Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwili wa Sista baada ya kupigwa risasi leo June 23, 2014,tukio lililotokea eneo la Ubungo-Darajani karibu na River Side Jijini Dar es Salaam.


Hali ya hewa imechafuka kwa wakazi wa eneo la Ubungo-Darajani karibu na River Side Jijini Dar es Salaam ,baada ya majambazi kumuua Sista wa Parokia ya Makoka-Mwisho aliyefahamika kwa jina moja la Kapuli na kisha kumjeruhi dereva wa gari na kutokomea na mkoba wa marehemu kusikojulikana.

Tukio hilo la kinyama limetokea majira ya saa 7 na nusu leo June 23,3014,mchana wakati sista huyo aliyekuwa na dereva wakitokea benki kufika eneo hilo kwa lengo la kununua mahitaji muhimu.

Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni dereva wa gari aliyefahamika kwa jina la Mark Patrick Mwarabu alisema kuwa marehemu alishangaa kuona amezungukwa na watu watatu waliokuwa wameshuka kwenye pikipiki aina ya Boxer na kumfuata kisha kumpiga risasi kadhaa.

Aliongeza kuwa, marehemu alikuwa ameenda kulipia pesa kwa ajili ya kununua mchele kwenye duka moja la nafaka kabla ya kuvamiwa na majambazi hao waliompiga risasi na kutokomea na mkoba wake huku wakimpiga risasi dereva huyo kidoleni.

(HABARI/PICHA: Deogratius Mongela / GPL).


Kidole cha dereva kilichokatwa kwa risasi.

Ganda la risasi likiwa eneo hilo la tukio.

Gari alilokuja nalo marehemu Sista Kapuli.

...Dereva akiwasiliana na jamaa zake baada ya kupigwa risasi na sista aliyekuwa naye kuuawa.

Gari lenye namba za usajili T 213 CJZ alilokuja nalo Marehemu.

Mwili wa sista ukiingizwa kwenye gari la polisi.


Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakichukua matukio eneo hilo la eneo la Ubungo-Darajani karibu na River Side Jijini Dar es Salaam

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top