Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
luisss
Mchezaji wa Uruguay Luis Suarez atakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kwa muda mrefu kucheza mechi zikiwemo za Kombe la dunia ikiwa atakutwa na hatia ya kumng’ata mchezaji mwenzake wa Italia Giorgio Chiellini.

Shirikisho la soka duniani limeanzisha uchunguzi dhidi ya mchezaji huyo  baada ya kuonekana akimng’ata mchezaji wa Italia, Giorgio Chiellini wakati wa mechi yao ya kombe la dunia.
luis2
Chiellini amedai Suarez amemng’ata katika bega lake la kushoto lakini Suarez amejitetea kuwa mchezaji huyo alijigonga kwake.
Refari wa mechi hiyo hakuchukua hatua yoyote dhidi ya Suarez.

Ikiwa atapatikana na hatia, Suarez huenda akazuiwa kucheza mechi 24 au kwa miaka miwili.
Suarez mwenyewe tayari amejitetea katika vyombo vya habari nchini Uruguay.
Suarez anasema Kuna mambo fulani ambayo hutokea uwanjani na hadhani ni vyema kuanza kuzua kashfa kutokana na mambo kama hayo.
kama huja jiunga nasi kwenye  ukurasa wetu wa facebook kwa habari zaidi BONYEZA HAPA

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top