Mtoto Salum Kassim akiwa na maumivu makali ya kuvimba tumbo yaliyosababiswa na ugonjwa wa moyo.
“Eeh
Mungu sikia kilio changu unisaidie!” Ndivyo alivyoanza kusimulia mtoto
Salum Kassim (16), mkazi wa Kilimahewa-Tandika, Dar, ambaye ameteseka
kwa muda wa miaka minne (siku 1440) akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo.Akizungumza
kwa maumivu makali na wanahabari wetu nyumbani kwao maeneo hayo, Salum
alisema tatizo hilo la moyo limemsababishia matatizo mengine ya kiafya
kama moyo kujaa maji, kuvimba tumbo, kushindwa kuhema, kukaa vizuri,
kulala na kutembea.
Salum
alisimulia kuwa mateso anayoyapata kupitia ugonjwa huo yamemfanya
kushindwa kuendelea na masomo kwani aliacha akiwa darasa la tano katika
Shule ya Msingi ya Moma iliyopo mkoani Mtwara, hivyo kuanza kuhangaika
na matibabu hadi mwaka 2012 alipohamishiwa Hospitali ya Muhimbili, Dar
kwa matibabu zaidi.
Alisema
kuwa baada ya kufika Dar na kuanza matibabu, amejikuta akikabiliwa na
changamoto nyingi kwani kila kitu kwake ni shida kutokana na ugumu wa
maisha na kushindwa kupata matibabu ya ugonjwa wake achilia mbali
chakula na malazi.
Alieleza
kuwa kuna wakati anakosa dawa kutokana na baba yake ambaye anaishi naye
kukosa fedha ya kununulia dawa na zaidi amekuwa akipata msaada kutoka
kwa mama wa jirani.
Alisema kuwa kutokana na ugonjwa huo kuna baadhi ya vyakula alivyokatazwa lakini anakula kwa sababu ya ugumu wa maisha.
“Mara nyingine tunashindwa kwenda kufuata dawa kwa sababu baba mdogo anakuwa hana fedha.
“Ikitokea hivyo huwa ninakaa bila kuendelea na dozi hadi anapopata ndiyo naendelea,” alisema kwa uchungu.
Salum aliomba Watanzania wamsaidie ili apate matibabu na kurejea katika hali yake ya kawaida na kuendelea na masomo.
“Watanzania naombeni sana msaada wa hali na mali ili nipate matibabu ya huu ugonjwa kwani nimeteseka kwa kipindi kirefu.
Kaka wa
Salum aliyejitambulisha kwa jina la Issa Kassim aliwaomba wasamaria wema
kumsaidia mdogo wake kwa kwa hali na mali ili kunusuru uhai wake.
Kwa yeyote anayeguswa moyoni mwake na
anaweza kumsaidia mtoto Salum, awasiliane naye kupitia simu namba
0785999276 na 0682865248 ambazo ni za baba mdogo wa Salum aitwaye Kassim
au fika katika ofisi zetu za Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar.
Kutoa ni moyo si utajiri.
GPL
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment