Sakata la kusambaa picha zisizokuwa na maadili mitandaoni zikiwemo za watu maarufu hapa nchini leo limezungumziwa tena katika bunge la Tanzania kule Dodoma ambapo katika kipindi cha maswali na
majibu
Mhe. Habib Mnyaa ameonekana akihoji serikali inachukua hatua gani juu
ya watu wanaotuma picha zao zisizo na maadili mitandani zikiwemo za kina
Wema na Diamond wanazopiga wakiwa chumbani na kuweka kwenye mitandao.
Katika majibu yake waziri wa mawasiliano,
sayansi na teknolojia Prof. Makame Mbarawa anasema “Mhe. Spika kuhusu
picha zisizokuwa na maadili zinazowekwa katika mitandao na watu maarufu
na hata wasiokuwa maarufu serikali imeanza kuandaa kanuni zitakazokuwa
zikifuatilia Online Content ambapo itaanza kuchukua hatua baada ya
kufuatilia juu ya picha hizo na kuchukua hatua madhubuti”.
Baada ya kauli hiyo Spika wa bunge Mhe.
Anne Makinda alikazia akitaka majibu juu ya picha za juzi zilizosambaa
zikimuonyesha Mhe. Komba akiwa na binti mdogo ambazo mwenyewe alisema si
zake na wabunge kuonekana wakitaka majibu ambapo Mhe. Mbarawa anasema.
“Mhe. Spika kuhusu picha za juzi
zilizosambaa mitandaoni tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa
zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila tutachukua hatua
tutakapobaini zilipotoka.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment