Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
SAA
chache baada ya kamati ya Rufani ya shirikisho la kandanda Tanzania,
TFF, chini ya mwenyekiti wake, Wakili Julius Mutabazi Lugaziya
kumrudisha, Michael Richard Wambura kwenye uchaguzi wa Simba sc, mgombea
huyo amesema sasa haki imetendeka na uchaguzi utakuwa wa amani.
Wambura
amezungumza na mtandao huu dakika chache zilizopita na kusema kuwa
anaufananisha ushindi wake kama mchezo wa mpira wa miguu.
“Mpira wa
miguu una mechi ya nyumbani na ugenini, unaweza ukafungwa ugenini,
ukashinda nyumbani, bila kujali umeshinda goli ngapi, lakini ninachoweza
kusema ni kwamba haki imetendeke, matokeo yametoka, tujipange kwenda
kwenye uchaguzi ili wanasimba wapate viongozi wao wanaowataka”. Amesema
Wambura.
Mgombea huyo ameongeza kuwa hiki sio kipindi tena cha kutafuta mchawi, bali ni kipindi kinachohitaji wanasimba kuwa makini.
“Ni
kipindi cha kuwa makini, kuweka sera zetu hadharani, malengo yetu
hadharani, ili wana Simba wapate fursa ya kuchagua kwa sera, nadhani
hilo ndio ombi langu”. Ameongeza Wambura.
Hata
hivyo, Wambura amesema kesho ataongea na waandishi wa habari makao makuu
ya klabu ya Simba mtaa wa Msimbazi, kariakoo jijini Dar es salaam.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment