Wakazi wa Zanzibar wako katika hali ya wasiwasi baada ya kushuhudia tukio lengine la kulipuka bomu kwa viongozi wa dini huku safari hii likiua kijana mmoja na kujeruhi saba.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa upelelzi na makosa ya jinai zanzibar
Sacp Yussf Ilembo, bomu hilo lilitupwa na mtu au watu
wasijulikana ambao walikuwemo ndani ya gari lilkuwa halina namba za
usajili ....
Ilembo amesema kuwa bomu hilo lilitupwa kwa kikundi cha wananchi waliokuwa pamoja na
viongozi wa dini ambao walikuwa wametoka msikitini na wamesimama nje ya
gari.
Kijana mmoja Mohamed khatibu
Mkombalaguha ambaye ni mkaazi wa pongwe Tanga aliyekuja Zanzibar kwa
ajili ya hitima alifariki hapo hapo na wengine saba akiwemo Sheik Kassim
Mafuta wamejeruhiwa...
Nao baadhi ya majeruhi Ahmed Haidar na mwanawe khalid Ahmed
wakiongea wakiwa wamelazwa hosptali ya Alrahma wamesema hawajui
wala hawakumuona mtu ailyerusha bomu hilo, wao wameshtukia mlipuko
mkubwa .
Mkurugenzi huyo wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar
amesema kuwa jeshi la Polisi limeanza kuwasaka waliohusika na mlipuko wa
bomu hilo.
source: TBC
source: TBC
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment