Mtoto
Melina wa (15) aliyefika katika Jiji la Dar es Salaam mwaka 2012
akitokea kijijini Ishozi- Kiziba, Kagera kwa lengo la kufanya kazi za
ndani, yaani ‘hausigeli’ akiwa amejeruhiwa vibaya na bosi wake
anayefahamika kwa jina moja la Yasinta.
SIKU 730 au
miaka miwili ya unyama na ukatili uliombatana na vipigo mfululizo,
vimempa wakati mgumu katika maisha mtoto wa miaka 15, Melina aliyefika
katika Jiji la Dar es Salaam mwaka 2012 akitokea kijijini Ishozi-
Kiziba, Kagera kwa lengo la kufanya kazi za ndani, yaani
‘hausigeli’Melina amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi) ya Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar baada ya kujeruhiwa vibaya usoni na
kichwani na bosi wake anayetajwa kwa jina moja la Yasinta ambaye ni
mwanasheria mkubwa nchini.
Tukio
hilo la kusikitisha, lilijiri Ijumaa iliyopita nyumbani kwa mwanamke
huyo, Boko-Magengeni jijini Dar ambako Melina alikuwa akifanyia kazi.
Binti
huyo ambaye wakati anafika jijini Dar alikuwa na miaka 12, licha ya umri
wake kuwa mdogo alifanya kazi kwa bidii ili mshahara wake uweze
kuwasaidia wazazi wake ambao hawajiwezi kimaisha kule kijijini.
SAKATA ZIMA LA MELINA
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Melina alichukuliwa na bosi wake huyo kwa
makubaliano ya mshahara wa shilingi 40,000 kwa mwezi huku shilingi
20,000 zikitumwa nyumbani kwao Kagera.
“Lakini
katika hali ya kushangaza, bosi wake alikuwa hampi zile shilingi 20,000
kama makubaliano yao yalivyokuwa akisema kwamba anamtunzia kuepuka
matumizi mabaya.
“Ikaelezwa
kuwa, akiwa ndani ya kazi, binti huyo alijikuta akipata mateso makubwa
kama vile kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kwa madai ya kukosa,
kufanya kazi vibaya au tofauti na maelekezo,” kilisema chanzo.
Melina
akiendelea kuuguza majeraha akiwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi) ya
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar baada ya kujeruhiwa vibaya usoni
na kichwani na bosi wake.
BINTI MWENYEWE ANASIMULIA
Akizungumza kwa uchungu akiwa hospitalini hapo, Melina anaanza kwa kusema:
“Nimechoka sana ndugu zanguni, nimeteseka sana, nisaidieni nirudi
kwetu Kagera. Kosa dogo napigwa na blenda na nyaya za kompyuta. Ndiyo
maana sehemu mbalimbali za mwili hadi kichwani nina makovu kama hivi.
“Mara hii ya
mwisho nilipigwa na kwanja la kufyekea ndiyo majeraha haya. Wakati
akinitesa bosi wangu alikuwa akiniambia hakuna wa kumtisha. Nisaidieni
jamani, miaka miwili ya mateso mfululizo sasa nataka kurudi kwa wazazi
wangu japokuwa hawana uwezo tutaishi hivyohivyo tu. “
MAKOVU 73 KICHWANI, MWILINI
Mbali na majeraha mapya, mtoto huyo ana makovu (majeraha yaliyopona)
73 kichwani na mwilini mwake ambayo yote yanadaiwa yalitokana na adhabu
ya mashambulizi ya kudhuru mwili ingawa haikubainika kama ni kutoka kwa
bosi wake huyo au la!
SIKU YA TUKIO
Juni 11, mwaka huu, saa 3 usiku, Melina alipelekwa katika hospitali
binafsi iliyopo Mbezi, Dar akiwa na majeraha makubwa kichwani.
Aliambatana na wanawake watatu, mama Betty, mama Winnie na mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Rwechungura.
Walisema
wao ni majirani wanaoishi karibu na binti huyo na walifika hospitalini
hapo kwa lengo la kumsindikiza na kujua nini kinaendelea.
DAKTARI NA MELINA
Habari zinadai kuwa, daktari aliyekuwa zamu usiku huo alishtushwa na
hali ya Melina kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi usoni na kichwani.
Aliwatoa wanawake hao nje na kumuuliza Melina nini kilimpata ambapo alijibu: “Nilianguka na ndoo ya maji.”
Daktari
alimbana sana ndipo akapasua jipu kwamba alikuwa amepigwa na bosi wake
na kwamba hata makovu mengine ni majeraha yaliyopona ambayo yalitokana
na kipigo cha mara kwa mara.
DAKTARI AOMBA NAMBA ZA SIMU
Ikadaiwa kuwa, daktari huyo aliomba namba ya simu ya mmoja wa wale
wanawake lakini walikataa na kumuomba daktari atoe yake wao ndiyo
wangempigia.
SAKATA LATINGA POLISI
Habari zinazidi kudai kuwa, daktari huyo aliendelea kuokoa maisha ya
Melina kwa kumshona nyuzi karibu kumi na mbili katika maeneo
yaliyopasuka lakini kutokana na hali ya majeruhi kuwa mbaya, ilibidi
aende kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe.
“Polisi
walikwenda nyumbani kwa mwanasheria huyo, lakini katika hali isiyokuwa
ya kawaida walikuta nyumba haina mtu tena ikiwa wazi kwa usiku huo.
“Inasemekana
katika wale wanawake watatu waliompeleka Melina hospitali, mtuhumiwa
alikuwepo ila alitoroka baada ya polisi kuonesha nia ya kumkamata.
“Hali ya
Melina ilizidi kuwa mbaya. Alfajiri ya Juni 12, mwaka huu ilibidi
ahamishiwe kwenye Hospitali ya Mwananyamala ambapo alipokelewa na kupewa
matibabu. Hali ikazidi kuwa mbaya, akahamishiwa Muhimbili.
POLISI WAKIRI, WAMKAMATA MTUHUMIWA
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura alikiri
kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kwamba, mtuhumiwa alitoroka lakini
Jumamosi iliyopita alitiwa mbaroni maeneo ya Mbagala jijini Dar.
NI HAUSIGELI WA PILI
Tukio la Melina ni la pili, wiki mbili zilizopita, hausigeli
mwingine, Yasinta Lucas alikumbwa na kadhia kama hiyo. Yeye alilazwa
Hospitali ya Mwananyamala akidaiwa kuteswa, ikiwemo kung’atwa meno na
bosi wake kwa kumtuhumu kutofanya kazi vizuri.
Bosi huyo
alishapandishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar, Juni
12, mwaka huu na kusomewa mashitaka ya kujeruhi.
Credit GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro











Post a Comment
Post a Comment