Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
INGAWA Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema itatangaza kesho mchana uamuzi wa Rufaa ya Mgombea wa Urais wa Simba SC, Michael Richard Wambura, lakini habari zisizo rasmi zinasema gwiji huyo amerudishwa kwenye mbio za kuwania uongozi wa Wekundu wa Msimbazi. 
  Wakili Julius Lugaziya ameambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba; “Tumemaliza, lakini tutakuwa na mkutano kesho mchana kutangaza uamuzi, kwa sasa huwezi kupata habari yoyote, tumekubaliana hivyo, yote yatatajwa kesho,”.      
 Amerudishwa? Habari zisizo rasmi zinasema Wambura amerejeshwa, lakini Kamati ya Rufaa itakuwa na Mkutano kesho na Waandishi wa Habari kutaja hukumu Majibu kama hayo yametolewa pia na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo, aliyesema; “Uamuzi kuhusu rufani ya Michael Wambura kupinga kuenguliwa kugombea urais wa Rais utatangazwa kesho (Juni 11 mwaka huu) saa 6 kamili mchana na Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Julius Lugaziya,”.

Lakini kwa mujibu wa habari za kiuchunguzi ambzo BIN ZUBEIRY imezipata ni kwamba baada ya mlolongo wote tangu jana Saa 5:00 asubuhi hoteli ya Courtyad, Upanga, Dar es Salaam hadi jioni ya leo, Wajumbe wa Kamati hiyo waliamua kupiga kura kuamua na Wambura akapata kura tatu kati ya tano za kumkubalia aendelee na mbio za Urais Simba SC. Wambura alikata rufaa TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kumuengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC chini ya Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro ilimuengua Wambura kwa sababu alikiuka Katiba ya klabu hiyo, TFF na FIFA kwa kuipeleka klabu hiyo mahakamani.
Chanzo BIN ZUBEIRY 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top