Dokta Herman akitahayali baada ya tukio hilo.
Dokta mmoja aliyefahamika kwa jina la Herman amenaswa katika dispensari moja iliyopo Buguruni Kwamnyamani jijini Dar akijiandaa kumtoa mimba mwanafunzi.
Awali,
kikosi kazi cha kufichua maovu cha Global Publishers (OFM), kilipewa
malalamiko juu ya dispensari hiyo kuwa ni kinara wa mchezo huo mchafu wa
kuwatoa mimba mabinti wadogo hususan wanafunzi wa shule za msingi.
Siku aliyonaswa, ilikuwa majira ya jioni
ambapo kaka wa mwanafunzi (jina tunalihifadhi) aliandaa mtego wa kumnasa
daktari huyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa rafiki wa mdogo wake
kuhusu mchezo huo mchafu anaoufanya daktari huyo.
Kaka huyo aliwapigia simu makamanda wa OFM
ambapo walitia timu sambamba na polisi kwenda kuweka ‘kambi’ katika
dispensari hiyo kuhakikisha tukio zima linakuwa ‘recorded’.
Kaka huyo alitanguliwa katika dispensari
hiyo na kubana sehemu kumsubiri mdogo wake huyo afike ‘kutoa mimba’ huku
makamanda wa OFM wakiwa wameseti mitambo yao maalum katika kila engo ya
eneo hilo.
Majira ya saa tisa, mwanafunzi huyo alifika
hapo akiwa ameongozana na kijana mmoja aliyesetiwa kuwa mpenzi wa
mwanafunzi huyo na kuongea jambo (kumpa fedha) na daktari akiingia
chumbani akiongozana na mwanafunzi huyo huko akiwa na vifaa maalum vya
kutolea mimba.
Nesi,dokta chini ya ulinzi.
Baada ya kusubiri kwa dakika tano, kaka wa
mwanafunzi huyo na makamanda wa OFM waliingia katika chumba hicho na
kumkuta daktari huyo akiwa katika pilipilika za kumtoa mimba mwanafunzi
huyo ambaye alikuwa amelala chali.
OFM ilifanikiwa kunasa meseji mbalimbali za daktari huyo zilizokuwa zikielekeza namna ya kufanikisha zoezi hilo la utoaji mimba.
Majirani ambao walishuudia tukio hilo
walipongeza sana OFM kwa kumnasa daktari huyo kutokana na kukithiri kwa
tabia hiyo dispensarini hapo.
”Jamani mmefanya vizuri sana kuja kukomesha
mchezo huu hapa tumelalamika sana lakini hatusikilizwi,” alisema mzee
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la mzee Hamisi.
Daktari huyo alipelekwa katika kituo kidogo
cha polisi cha Buguruni kisha kuchukuliwa maelezo ili hatua zaidi za
kisheria dhidi ya daktari huyo ziendelee.
Mpaka timu ya OFM inaondoka eneo la tukio
hilo, walimuacha daktari huyo akiwa anashikiliwa kituoni hapo na shauri
lake likisomeka MNY/RB/336/2014.
Credit GPL
kama huja like ukurasa wetu wa facebook kwa habari zaidi BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro










Post a Comment
Post a Comment