Wakati
macho na masikio ya dunia yote yakiwa kwenye soka hasa kwa kipindi hiki
cha kombe la dunia sasa inshu imekuwa tofauti kwa kampuni ya Beats by
Dr.Dre ambayo headphone zake zimepigwa marufuku kutumika kwenye kombe la
dunia.kampuni ya Beats Electronics ilitoa tangazo la luninga lililokuwa
na dakika 5 ambalo walilipa jina la ‘Tittle the Game before the
Game’.
Katika tangazo hilo wapo mastar kadhaa wa mpira wa miguu kwa msimu
huu akiwemo mchezaji nyota toka Brazil Neymar Da Silva Santos
Júnior,Mchezaji wa Spain Francesc “Cesc” Fà bregas pamoja na mchezaji
kutoka Uruguay Luis Alberto Suárez DÃaz pamoja na Lil Wyne.Unaambiwa
baada ya FIFA kuliona hilo tangazo wamewakataza wachezaji wote kuvaa
headphones hizo za Beats by Dre wakiwa kwenye viwanja hivyo vya kombe la
dunia pamoja na sehemu zote za sherehe zitakazowahusisha pia waandishi.
Dili
limeidondokea kampuni ya Sony ambao ni Official Partner na FIFA ambao
wameahidi kuwapatia wachezaji hao headphones za kuvaa kwa kipindi hicho
cha kombe la Dunia na hawataruhusiwa kuvaa aina nyingine yoyote ya
headphone.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment