Mnenguaji wa
Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis akionyesha sehemu alikopigwa risasi
mbili mwilini na mtu aliyedaiwa ni askari polisi.
MNENGUAJI wa
Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis ambaye usiku wa Jumatano iliyopita
alipigwa risasi mbili mwilini na mtu aliyedaiwa ni askari polisi,
ameweka undani wa sakata hilo.
Akizungumza
na gazeti hili juzi nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, majeruhi
huyo alisema tukio hilo lilijiri maeneo ya Mwananyamala- Kisiwani karibu
na Ofisi za Chama cha Wananchi (Cuf) na kuongeza kuwa, kisa ni
kubishana na askari huyo aliyetaka kuzimwa kwa matarumbeta kutoka kwenye
kikundi chao kilichokuwa kikipita eneo hilo.
“Sisi
tulikuwa tukipita na matarumbeta, askari wakatusimamisha na kutuamuru
tuyazime kisha kutaka kutukamata watupeleke kituoni eti serikali
imekataza. “Tuliwaambia mbona ni mapema sana kwani ilikuwa saa kumi
alasiri na Kova alisema ngoma za Kanga Moko, Kigodoro na nyingine
zisipigwe usiku. Pia tuliwaambia tulichokuwa tukikifanya si ngoma hasa,
ni matarumbeta tunapita kuwaalika watu kuwa leo kuna shughuli sehemu.
Mnenguaji wa Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis akiwa hoi kitandani baada ya kujeruhiwa na risasi.
“Baada
ya majibu hayo ndipo askari mmoja hakutaka hata kuendelea na
mazungumzo, alitoa bastola kiunoni na kunipiga risasi mbili, moja
kiunoni, nyingine kwenye mbavu halafu akapiga tena hovyo hewani risasi
zilizobaki. Kwa kweli nimeumia sana,” alisema Zawia.
Mnenguaji
huyo alisema kutokana na hali yake kuwa mbaya alipelekwa Kituo cha
Polisi cha Mwinjuma na kupewa Polisi Fomu No. 3 (PF3) kisha kukimbizwa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni, Mwananyamala kwa ajili ya
matibabu ambapo kwa mujibu wake alitolewa risasi mbili.Baada ya
kuzungumza na majeruhi huyo, waandishi wetu walikwenda kwenye Kituo cha
Polisi Mwinjuma ambako ndiko alikoripoti PF3.
Askari
mmoja wa kituo hicho (jina lipo) alisema hawezi kusema lolote kuhusu
tukio huku akiweka wazi kwamba, afande aliyempiga risasi mnenguaji huyo
anajulikana hivyo mlalamikaji anaweza kwenda mbele ya sheria.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Dar, Camillius Wambura hakupatikana kwa
simu juzi kuzungumzia tukio hilo lakini gazeti hili linaendelea
kufuatilia.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment