Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

TIMU ya Taifa ya Algeria imejiweka mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya 16 ya kombe la dunia baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya Korea kusini usiku huu.
Huu ni ushindi mzuri kwa Algeria hasa baada ya Urusi kufingwa bao 1-0 na Ubelgiji, hivyo wawakilishi hawa wa Afrika watahitaji pointi moja tu dhidi ya timu ya Urusi chini ya kocha Fabop Capello.
Mabao Algeria yamefungwa na Slimani katika dakika ya 26, Halliche 28, Djabou 38, Yacine Brahimi 62.
 Mabao ya Korea kusini yamefungwa na Son katika dakika ya 50 na Koo dakika ya 72.

Kikosi cha Korea kusini: Jung, Yun, Kim, Son, Park (Kim 58), Lee (Lee 65), Koo, Han (Ji 78), Ki, Lee, Hong
Kikosi cha Algeria: Mbolhi, Bouguerra (Belkalem 89), Halliche, Mesbah, Feghouli, Brahimi (Lacen 77), Medjani, Slimani, Bentaleb, Djabou (Ghilas 73), Mandi Goals: Slimani 26, Halliche 28, Djabou 38, Brahimi 62
Booked: Bouguerra

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top