Kituo
cha TV cha CNN ambacho kimeshinda tuzo kutokana na ubora wa kazi ya
kutangaza habari wanayoifanya toka kuanzishwa kwake mwaka 1980, kimetoa
ripoti ya Watu watatu wenye ushuhuda wa maisha yao ambao walikufa na
kuacha miili yao duniani, kisha wakaenda mbinguni na kurejea tena
duniani ambapo huyu hapa chini ni mmoja wao.
Mwanamke huyu Daktari aitwae Mary raia wa Marekani January mwaka 1999 alimchukua mume wake na kumzawadia safari ya kwenda Chile kusherehekea birthday yake ambapo walipofika nchini humo wakiwa na mpango wa kukaa kwa siku kadhaa walifanya kila walichopanga kufanya kwa siku hizo hivyo ikawa imebaki siku moja,yani siku ya mwisho ambayo mume wake aliamka akiwa anaumwa mgongo hivyo hakuweza kwenda kutembea na hizo boti mtoni kama kawaida yao.
Yani kuna zile boti ndogo za mtu mmoja mmoja ambazo unaingia unanyoosha miguu yako kwenye sehemu ya mbele alafu unaanza kuliendesha mwenyewe.
Kwa
sababu mume alikua anaumwa mgongo, mke aliamua kwenda kutembea mwenyewe
na boti siku ya mwisho… hata hivyo haikua sawa kwake pia, alikua kama
anasitasita lakini akaenda hivyohiyvo alafu akatembea na boti kwenye
sehemu yenye maporomoko makubwa ya maji, yenye umbali wa futi 10 mpaka
15 ambako boti yake ilizama kwenye moja ya maporomoko na akajikuta
amekwama katikati ya miamba chini ya maji.
Anasema alikua na uhakika kwamba anakufa kwa sababu alikaa muda mrefu kwenye maji hivyo akaamua kumuachia Mungu kila kitu na bada ya hapo tu akahisi kama muujiza, kuna nguvu imemkumbatia na ikawa inamuhakikishia kwamba kila kitu kitakua sawa kwa upande wa mume wake na watoto, hapo ndio akaamini mtu ambae anaamini ni Yesu Kristo alikua amemkumbatia.
Akawa
anajiuliza maswali kuhusu hiki kitu ambacho ni cha ajabu kwake,
alipoulizwa na Mtangazaji kama alikua anajitambua wakati akiwa mikononi
mwa Yesu, Mama huyu amekiri ndio alikua anajitambua mpaka alikua anaona
maji na bado pia alikua amebanwa kwenye boti.
Ghafla kila kitu kilibadilika akaona malaika wanajadiliana na Yesu, akaona wale waliokua wanamtafuta wameshaona jiwe ambalo halijukani lilitokea wapi ila halikuepo mwanzoni na kisha wakamuona yeye baada ya kulifata hilo jiwe, akasaidiwa na kutolewa akiwa ameshabadilika rangi kabisa.
Kwa
kawaida binadamu akikaa kwenye maji kwa dakika 10 anakufa ila yeye
alikaa kwa dakika 30 lakini akatoka akiwa hai lakini alikua
ameshabadilika rangi na kuvimba mwili pia ambapo anasema katika
mazungumzo yake na Yesu, kuna malaika mmoja alimwambia kwamba mtoto wako
atafariki siku kadhaa zijazo, na kweli mtoto alifariki wakati akiwa
kwenye michezo.
Kabla ya hapo mama huyu alikua anasita kumwambia mume wake lakini mtoto alivyofikisha miaka 18 ndio ikabidi amwambie kuhusu hizo habari za kifo.
Umemuamini huyu mama na hii stori yake?
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment