Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Bwana Gabriel Lyimo Nderumaki kuwa Mhariri Mtendaji wa
Kampuni ya Magazeti ya Serikali, Tanzania Standard NewsPapers (TSN).
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Mei, 2014.
Kabla ya uteuzi huo Bwana Nderumaki alikuwa Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Mei, 2014
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment