Mwili wa askari aliyeuawa ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Temeke
Askari polisi mmoja wa kituo cha polisi
Chang'ombe, Mkoa wa kipolisi wa Temeke, ameuawa kikatili siku ya ijumaa
mchana baada ya kupigwa risasi ya kifua na majambazi waliokuwa
wanajaribu kutoroka baada ya kufanya tukio la kihalifu. Askari hao
waliokuwa doria katika eneo la Wailes walijikuta wakishambuliwa kwa
risasi na majambazi hao mara baada ya majambazi hao kujaribu kukimbia
katika eneo la tukio kwa kutumia usafiri wa pikipiki kipindi ambapo
askari polisi walikuwa karibu na eneo la tukio. Hata hivyo wakati askari
hao wakijaribu kuwafukuza majambazi hao wawili kwa lengo la kuwakamata
ndipo jambazi mmoja alitoa bastola na kumpiga risasi ya kifua askari
huyo na kufariki pale pale.
Mwili wa askari huyo ukiwa umehifadhiwa.
Hata hivyo katika harakati za
kujaribu kukimbia majambazi hao walianguka na pikipiki waliyokuwa
wakitumia ndipo wakaamua kutimua mbio mitaani na kuingia katika nyumba
moja ambapo walijificha na kujifanya kama ni wakazi wa eneo hilo, baada
ya wnanchi na polisi kufika katika nyumba hiyo, baadhi ya majirani
waliwaambia polisi kwamba wameona watu hao wameingia katika nyumba hiyo.
Baada ya polisi kuingia waliwakuta watu hao wakiwa wametulia kama
kwamba wao ni wakaazi wa nyumba hiyo na wala hawajui lililotokea.
Mwili wa mmoja wa majambazi ukiwa chumba cha kuhifadhia maiti
Baada ya kuwatambua watu hao,
polisi waliwatia nguvuni huku wananchi wenye ghadhabu waking'ang'ania
kuwa wanataka kuwaua sababu wameshaua askari mmoja. Baada ya vuta
nikuvute kati ya wananchi na askari hao ambao walikuwa wachache,
wananchi walifanikiwa kuwachukua majambazi hao kwa nguvu kutoka mikononi
mwa polisi na kuanza kuwapiga kwa silaha mbalimbali za kienyeji
yakiwemo mawe na marungu mpaka watuhumiwa hao wakapoteza maisha.
Mwili wa jambazi mwingine ukiwa umeharibika vibaya baada ya kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira.
Mwili wa askari polisi ukiwa umepakiwa kwenye gari ya polisi tayari kupelekwa hospitali ya Temeke kuhifadhiwa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
waliiambia blogu hii kwamba majambazi hayo kabla ya kupambana na polisi
walikuwa wamefanya uvamizi na kumuibia mwanamke mmoja mkazi wa eneo
hilo. Hata hivyo mali au fedha iliyoibiwa haikuweza kujulikana mara
moja.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment