Watu
watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliohusika na utekaji na
unyan'ganyi wa gari Mei 12 mwaka huu eneo la Mlima Msangamwelu Wilaya ya
Mbeya Vijini wameuawa na wananchi katika mapambano makali pembezoni mwa
Mlima Mbeya.
Jambazi
la kwanza lilitambuliwa kwa jina la Kitwana Lugoya(30)mkazi wa Ilemi
Juhudi Jijini Mbeya ambaye aliuawa na wananchi baada ya kupata taarifa
ambapo walifanikwa kumzingira na kufanikiwa kumkamata eneo la
Msangamwelu Kata ya Mshewe.
Juhudi za
wananchi ziliendelea kwa kushirikiana na Jeshi la kuwasaka majambazi
wengine ziliendelea na kufanikiwa kuwakamata majambazi wengine wawili
waliotambuliwa kwa majina ya Ndayobi Lutego(26)mkazi wa Igunga mkoani
Tabora na Idd Sadiki(29) mkazi wa Veta Jijini Mbeya.Hata hivyo juhudi za
wananchi ziliendelea kuwasaka majambazi wengine wawili waliosalia
wakiwa na bunduki na risasi kadhaa ambao walitokomea katika msitu mnene
kupandisha Mlima Mbeya na kufanikiwa kukamata jambazi jingine lililokuwa
na silaha na mfuko wa risasi ambapo wananchi walilidhibiti ndipo
alirusha silaha na risasi msituni na kuanza kupambana na wananchi kwa
kusaidiana na Askari na kufanikiwa kumkamata na katika mapambano hayo
jambazi hilo liliuawa kwa kutumia silaha za jadi na mawe.
Jambazi
mwingine alikamatiwa katika Kitongoji cha Lunji Kijiji cha Ihombe kwa
ushirikiano na wananchi wa vijiji vya Ihombe,Iziwa,Ikukwa na Msangamwelu
ambalo pia lilipambana na wananchi hao na Askari majira ya saa tano
asubuhi Mei 13 mwaka huu ambapo lildhibitiwa na kuuawa.Mapambano hayo ya
hatari katika msitu huo yalikuwa yakifanyika kwa tahadhari kubwa
kutokana na kutojua idadi yao na aina ya silaha walizo nazo na mpaka
sasa silaha na risasi havijapatikana katika msitu huo.
Baadhi ya
majambazi kabla ya kuuawa imedaiwa kujihusisha na matukio ya ujambazi
wa kutumia silaha katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Njombe,Iringa
na Morogoro ambapo walikuwa wakitafutwa kwa muda mrefu na Jeshi la
Polisi.
Jeshi la
Polisi limewashukuru wananchi waliojitolea kupambana na majambazi hao
kwa kutumia dhana ya Polisi Jamii na ulinzi shirikishi ambayo imeanza
kuzaa matunda na kufanikiwa kukomesha vitendo vya uhalifu Mkoani Mbeya
ili Mbeya iwe na amani muda wote.
Wakati wa
uporaji majambazi hayo yapatayo matano yalipanga mawe barabarani eneo
la Msangamwelu na kufanikiwa kupora pesa,simu na pikipiki aina ya SANYA
yenye namba T 682 CHT ambayo baadaye waliitelekeza msituni walipokuwa
wanafuatiliwa na wananchi.
Majambazi
hao walimjeruhi Dereva wa roli hilo aliyefahamika kwa jina la Sephen
Mgogo ambaye amelazwa katika Hospitali Teule ya Ifisi na miili ya
majambazi hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya ambapo
wawili kati yao hawajatambuliwa.
Jeshi la
Polisi waliondoka Kijiji cha Ihombe majira ya saa moja na nusu usiku
baada kazi ngumu ya kubeba miili ya majambazi hao mwendo wa masaa matano
kwa miguu kutoka uneo la mapambano.
Na Ezekiel Kamanga wa mbeya yetu
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment