Marehemu Maximilian John Ngube enzi za uhai wake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari Mheshimiwa
Dkt.Fenella Mukangara kufuatia kifo cha Mpiga picha wa kituo cha television cha Mlimani, Ndugu Maximilian John kilichotokea alfajiri ya kuamkia leo tarehe 24 Mei,2014.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Bwana Maximilian
kilichotokana na maradhi ya Moyo, Sukari na Shinikizo la damu. Kifo hicho ni pigo na pengo kubwa kwa tasnia ya habari hapa nchini,”Amesema Rais Kikwete katika salamu hizo.
kilichotokana na maradhi ya Moyo, Sukari na Shinikizo la damu. Kifo hicho ni pigo na pengo kubwa kwa tasnia ya habari hapa nchini,”Amesema Rais Kikwete katika salamu hizo.
“Bw.
Maximilian atakumbukwa kwa uchapakazi wake na uhodori katika kazi zake
siku zote. Kifo ni maandiko ya Mwenyezi Mungu hivyo hatuna budi
kumshukuru kwa yote.
“Nakutumia
salamu zangu za dhati kuomboleza msiba huu. Aidha, kupitia kwako,
naitumia familia ya Ndugu Maximilian, pole za dhati ya moyo wangu kwa
kuondokewa na mzazi na mhimili wa familia. Aidha, salamu hizi ziwafikie
pia wanahabari wote, wafanyakazi wenzake, ndugu, jamaa na marafiki wa
marehemu. Nakuomba uwajulishe kuwa naelewa machungu yao katika kipindi
hiki na nawaombea subira na uvumilivu.
Ninaungana
nao kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya
marehemu. Amen,” amesema Rais katika salamu hizo.
Ndugu Maximilian John ameacha mke na watoto wanne.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Mei,2014
24 Mei,2014
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment