Majeruhi
bi Happiness Chacha (22) akiwa amelazwa katika wodi namba 8 katika
hospitali ya wilaya ya Geita baada ya kuungua moto yeye na mme wake
Majeruhi Chacha Wambura (35)akiwa amelazwa katika wodi namba 7 katika wilaya ya Geita baada ya kuungua moto katika kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita mkoani Geita.
Wanandoa
wawili wakazi wa kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita mkoani Geita
Happiness Chacha(22) na mme wake Chacha wambura(35) wamenusurika kufa
baada ya nyumba yao kuungua moto katika kibanda chao cha bar.
Tukio
hilo limetokea jana usiku saa nane usiku katika kijiji cha Lwamgasa
ambapo kufuatia tukio hilo majeruhi wakikimbizwa katika hospitali ya
wilaya ya Geita mkoani Geita walipolazwa wodi namba 7 na 8.
Robina
Isack anayewauguza amesema kuwa usiku huo wa saa 8 waliona moto unawaka
bila kujua umeanzia wapi huku wakishangaa kwa vile hawatumii nishati
hiyo ya umeme na wala hapakuwa na moto waliokuwa wamewasha ndani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Na Valence Robert-Geita
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment