Maria Said mama
mkubwa wa Nasra, katikati ni baba mzazi wa Nasra, Rashidi Mvungi, na
kulia ni mume wa Mariam Said wakiwa katika ofisi za ustwawi wa jamii
mjini Morogoro baada ya kukamatwa na kufikishwa polisi kwa tuhuma za
kumficha mtoto huyo ndani ya box kwa miaka 4 baada ya mama wa mtoto
huyo kufariki dunia kwa ugonjwa wa malaria .
Muuguzi katika
Wodi ya watoto hospitali ya rufaa ya Morogoro akimuhudumia mtoto Nasra
Said mara baada ya kufikishwa hopsitalini hapo kupatiwa matibabu.
Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.
MUME na mke wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumficha mtoto kwa miaka 4 ndani ya Box .
Kamanda
wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema tukio hilo lilibainika
Mei 20 mwaka huu majira ya saa 4.45 Asubuhi katika eneo la mtaa
Azimio kata ya Kiwanje Ndege Morogoro.
Alisema
majirani walizingira nyumba ya mwanamke ajulikanae kwa jina la Maria
Said na kutaka kuvunja ndipo polisi walipopata tarifa na kufika katika
nyumba hiyo na kukuta mtoto huyo akiwa katika box.
Alimtaja
mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Nasra Rashid Mvungi mine na nusu
ambapo polisi ilichukua jukumu la kupeleka kesi hiyo Ustawi wa jamii
ili kuendela nayo.
<<<<<BOFYA HAPA ULIKE PAGE YETU>>>>>
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment